Dear Mange,
Natumai unaendelea vizuri na majukumu ya kusukuma gurudumu la maendeleo
mbele.
Ni muda sasa tangu uje kunisapot kwenye kipindi changu cha Wanawakelive.
Nimekuwa nikikupgia simu yako ili nikushukuru kwa sapot uliyonipa kwani
kwa kufanya na wewe kipindi uliniongezea watazamaji wengi mno, na hiyo ni
kutokana na umaarufu mkubwa uliojijengea. Hakika wewe ni mwanamke wa
kipekee kabisa asante sana.
*Kwanini nimekuandikia*
Nilikuwa likizo ya uzazi kwa muda wa miezi mitatu, na katika kipindi hicho
nimekuwa nikirusha vipindi nilivyovirekodi nikiwa mjamzito, sasa
nimemaliza likizo najiandaa kurudi kwa hiyo ndo naandaa vipindi vipya.
Leo 28/5/2013 tutarudia kurusha kipindi chako kwenye EATV. Pia nimeona
umeanza biashara, binafsi nakupongeza sana na ninakukaribisha sana kwenye
kipindi kwa mara nyingine tena ili uje tuongelee bongolicious.
Sina la zaidi isipokuwa nakuombea Mwenyezi Mungu mambo yako yoooote yaende
kama unavyotarajia.
Asante sana.
OMG GUYS,
This email almost had me in tears. Haki ya Mungu i never expected Joyce to ever write to me to say thanks kwa lolote lile, especially ukiangalia kuwa comments zenu hazikuwa very friendly.....lol..... Lakini aliangalia kama challenge wala haikumsumbua......
Aisee kwenye maisha yangu sijawahi kumuweka mtu kwenye hii blog yangu na baadae akarudi kuniambia ahsante na akakubali kuwa this blog really helped them. Nimezoea kupewa shukurani ya mapunda (mateke) .This is the very first time someone
actually said 'THANKS'.
Omg, Joyce umenigusa. Although huwa nakataaga radio and tv interviews nikiwa bongo kwako ni big yeeeess, siku ntakayotua bongo nitakuja wanawake live for another interview............Nimekupenda bure Joyce... Shukrani ni kitu kidogo sana sana sana....
Kwa wale ambao hakuonaga ile interview yangu on wanawake live here you go.
WANAWAKE LIVE HUONYESHWA KWENYE EATV kILA JUMANNE SAA TATU USIKU....
part 1
Part 2
Part 3
Hiyo clip ya tatu imenikumbusha ahadi yangu moja that i didnt keep...... Duh, through bongolicious ntaanza kuifanyia kazi....